Update:

Wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba ya jijini Dar Es Salaam wasikitishwa na kitendo cha kupokonywa point 3 na kufungiwa kwa msemaji wa timu hiyo Haji Manara

Na Clement Shari
 Image result for Wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba


Wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba ya jijini Dar Es Salaam wamekuwa na maoni tofauti juu ya timu yao kupokwa pointi 3 walizopewa hapo awali na pia kufungiwa kwa msemaji wa klabu hiyo Haji Manara ambaye amefungiwa kwa mwaka mmoja na kutozwa faini ya shilingi milioni 9.

Mashabiki hao wamesema wamesikitishwa na yaliyotokea lakini wakasema wanautaka uongozi wa klabu yao kuelekeza nguvu zao kwa michezo mitatu iliyosalia na ule wa kombe la TFF ili timu yao iweze kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa msimu ujao.

Ama kwa upande mwingine mashabiki hao wamelilaumu shirikisho la soka humu nchini kwa kufanya maamuzi mara mbilimbili hali inayopelekea ladha ya soka kupungua

Mashabiki hao wamewataka viongozi wa klabu hiyo jijini Dar kuhakikisha wanalisimamia swala la Haji Manara kwa kukata rufaa ili haki itendeke.

No comments