Update:

Wajumbe wa kamati ya pili kuchunguza mchanga wa madini waapishwa

Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John 
Rais John Pombe Magufuli, amewaapisha wajumbe wa Kamati Maalum ya pili ya wachumi na wanasheria itakayochunguza mchanga wenye madini ulio katika makontena yaliyopo maeneo mbalimbali nchini.
 

Walioapishwa leo Ikulu, jijini hapa ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa Nehemiah Eliachim Osoro na wajumbe wake ambao ni Profesa Longinus Kyaruzi Rutasitara, Dk Oswald Joseph Mashindano.
 

Akizungumza baada ya kuwaapisha wajumbe wa kamati hii, Rais Magufuli amesema ameunda kamati hiyo ili ifanye uchunguzi wa kina utakaobaini aina ya madini yaliyo ndani ya mchanga huo, thamani yake, kiwango cha kila aina ya madini, uzito wa mchanga unaowekwa ndani ya makontena na pia kujua ni makontena mangapi yamepitishwa tangu mwaka 1998.

Wajumbe wa kamati ya pili kuchunguza mchanga wa madini waapishwa -... mkafuatilie tujue zimepelekwa tani ngapi za dhahabu, tani ngapi za shaba na tani ngapi za silva, je makontena mangapi yanapita kila mwezi? Makontena 1,000 au mangapi? na je zilikuwa na thamani ya kiasi gani? Je tumelipwa kiasi gani cha fedha?

No comments