Update:

Utoaji wa elimu bure wasaidia kudhibiti matumizi mabaya ya fedha.

Humphrey  Polepole  amesema kuwa utoaji wa elimu bure ya msingi na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali katika sekta  ya utumishi wa umma  na mageuzi ya muundo wa Chama zimelenga  kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma.
 Polepole  ametoa ufafanuzi huo kufuatia  baadhi ya wanachuo kutoka Shirikisho la Vyuo Vikuu (UVCCM) Mkoani Tabora  wakati wa kongamano la kuomba erikali kuongeza kasi ya utoaji vibali vya ajira katika sekta ya umma, fedha kwa ajili ya mafunzo ya vitendo kwa wanachuo na kuongeza wigo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali  nchini .
 Amesema  utoaji wa elimu bure ni sera ya kitaifa ya kiserikali ambayo inatakiwa kila mdau ashiriki kikamilifu ili kuhakikisha kila mwananchi  anapatiwa elimu stahiki.

No comments