Update:

UTI isihusishwe na Ngono


Mkojo mchafu (UTI) ni matatizo yanayotokea kwenye njia ya mkojo ambayo huchangiwa na maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Matatizo ya UTI husababishwa na vimelea (bacteria) ambavyo huingia katika njia ya mkojo. Ugonjwa huu huweza kumpata mtu yeyote pasipo kujali jinsia.
Hata hivyo, mwanamke huweza kuhisi dalili za UTI mapema zaidi kuliko mwanaume hii ni kutokana na tofauti za kimaumbile. Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hususan mfumo wa njia ya mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na vimelea
Kuhusu suala la Ngono kua chanzo kikubwa cha UTI, ni dhana inayotokana na imani iliyojengeka kwa baadhi ya watu kwneye jamii.
Dr Isaac Maro amefafanua hayo kwa kupitia akaunti yake ya Instagram kwa maelezo yafuatayo.
1) Kwanza, inasemekana kwamba UTI inaambukiza – yaani kwamba unaweza kumwambukiza mwenzi wako. Tukizungumza kiujumla, UTI (maambukizi kwenye mfumo wa mkojo) hayaambukizi, hapa tunamaanisha huwezi kupata UTI kutoka kwa mwenza wako kama ungefanya naye mapenzi/ngono. ILA , kama UTI ya huyo mwenza wako ilisababishwa na ugonjwa wa ngono ( maana kuna UTI zinazosababishwa na magonjwa ya ngono kama chymadia au trichomoniasis – hii hutokea pale bacteria wanaposambaa kwenye urethra ) basi wewe utakuwa hatarini kupata hayo magonjwa ya ngono hadi pale mwenzi wako atakapotibiwa. Hivyo basi, kitendo cha ngono chenyewe hakiwezi moja kwa moja kusababisha UTI bali kinaweza kuchangia katika kusukuma bacteria (vimelea) kwenye mrija wa mkojo) na kusababisha muwasho katika hili eneo na hili linaweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata UTI.
2) Pili, inasemekana kwamba watu wanaofanya ngono ndio hao tu wanaopata maambukizi haya. Hapana, UTI inaweza kutokea wakati wowote maishani, hata kama mtu hajaanza kujamiiana – ingawa UTI inawatokea sana wanawake wajawazito, na watu wazima. Kujamiiana kunaweza kuamsha maambukizi ya mfumo wa mkojo lakini haumweki mtu kwenye hali ya hatari kupata maambukizi haya.
3) Tatu, kwenda haja ndogo baada ya ngono kunakinga maambukizi ya UTI. Hii ni kweli pale mtu anapokojoa haswa mpaka kibofu kinakuwa kitupu bila mkojo.
credit: bongo5

No comments