Update:

Siku ya Kimataifa ya Msichana na Tehama-TCRA kanda ya kasikazini yaazimisha na sekondari ya Longido-ARUSHA


Katika kuazimisha siku ya kimataifa ya msichana na Tehama,Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kanda ya kaskazini  imeiazimisha siku hiyo na wanafunzi wa shule ya sekondari ya longido mkoani Arusha kwa kuwahamasisha wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na technolojia ya Tehama na kutoa elimu ya mawasiliano ili kutumia mtandao kwa njia sahihi
 WANAFUNZI WA SHULE YA LONGIDO SEKONDARI WAKIWA KATIKA DARASA L KOMPYUTA

 Akizungumzia siku hiyo ya msichana na Tehama na  umuhimu wa wanafunzi kujifunza somo hilo,maneja wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya kaskazini Mhandisi Annet mahimbo matindi amesema kuwa,soko la Tehama linauhitaji wa watu wengi sasa na  lina fursa nyingi sana hasa kwa wanawake hivyo wasichana wanatakiwa kutokuogopa  masomo hayo ili kukutana na furusa nyingi za ajira
 
"Tumekuja hapa kukutana na wasichana wanaosoma katika shule hii ya longido sekondari,Tumewafahamisha umuhimu na faida za  TEHAMA,na pia tumewahamasisha wasiogope masomo ya sayansi kwasababu yana future nzuri"
MHANDISI ANNET MAHIMBO MATINDI AKIELEKEZWA NA WASICHANA NA SHULE YA LONGIDO JINSI WANAVYOSOMA COMPYUTA  JIJINI ARUSHA

Wakizungumzia siku hiyo ya wasichana,Baadhi ya wasichana wa shule ya longido sekondari wanasema wanashukuru mamlaka ya mawasiliano Kanda ya kaskazini kuwatembelea na kuwafundisha mengi kuhusu Tehama ila mbali na hayo wanachangamoto nyingi kama vitabu,walimu, vifaa vya kutosha vya kujisomea kama za kompyuta za watu wenye  walemavu wa macho

 "Tunawashukuru na tunafurahi TCRA kwa kututembelea shuleni kwetu leo na kuazimisha siku hii ya msichana na TEHAMA duniani kote,tunashukuru mmekuja kuongea na sisi ili kutupa hamasa zaidi kufanya vitu kuhusuna na tehama zaidi ili kupata kipato ama kujipatia furusa mbalimbali duniani kote,kwasababu ukisoma tehama unaweza kufanya kazi popote pale nchini na duniani serikalini au sekta binafsi"

"Na mkisimama hapa kama mnavyoona hawa ndo walimu wetu wawili wa tehama,hiki ndo chumba chetu ambacho tunatumia kuhusiana na TEHAMA japokuwa tunavifaa vichache lakini kidogo vinatusaidia na bhado wenye uoni afifu wanavifaa pia vichache kama mnavyoviona hapa,na tunawashukuru sana kuja shuleni kwetu tunawakaribisha tena  muendelee kututembelea na kuzidi kutuongezea hamasa na mtuongezee hata chumba kingine cha kompyuta ili viweze kututosheleza kwa idadi ya wanafunzi"

"wasichana wengi wamekuwa wakiogopa masomo ya sayansi wakikwepa kwamba wawanatumia muda mwingi wa kusoma,na hata hivyo si kwamba kukwepa kusoma tu hapana kama tukiangalia Tanzania yetu sasa ivi tunahitaji vitabu ambavo vitakuwa na muongozo wetu ,kwamba tunakitabu chetu cha kompyuta,vitabu ambavyo vinatakiwa vipatikane katika shule na hiyo ndo changamoto yetu kubwa ambayo ninaweza nikalia na serikali yetu,pili walimu wa tehama hawapewi kipaumbele kama walimu wengine"katibu wa shule hiyo Happyness Adolph Silayo  akizingumza

Kwa upande wao walimu wa Tehama wa shule ya secondary longido wameishukuru mamlaka ya mawasiliano kwa kuadhimisha siku hiyo shuleni kwao na kuwapatia vifaa,pia wameiomba serikali kuwatatulia changamoto kubwa walionayo hasa ya vitabu vya kufundishia tehama na kujaribu kuomba mtiani ya tehama kutugwa.
Aitha bi Annet ametoa rai kwa  wadau mbalimbali  na serikali kujitolea vifaa kama kompyuta na vitabu vinavyo kidhi mahitaji ya wanafunzii

No comments