Update:

RC ;GAMBO AMUAGIZA KAMANDA WA POLISI ARUSHA KUFANYA MSAKO WA KUWABAINI WANAO TUMIA UMEME KINYAMELA WAKAMATWE

Displaying IMG_20170429_114309.jpgWakati shirika la umeme nchini TANESCO likiendelea na jitihada za kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya umeme taasisi pamoja na mashirika mbalimbali mkoani Arusha wametakiwa kuhakikisha wanalipa bili zao za umeme kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa.

Agizo hilo limetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo katika ziara yake anayoendelea nayo jijini hapa ambapo ameeleza kuwa yapo mashirika pamoja na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanalipa bili zao za umeme kutokana na kuwapo kwa mashirika mbalimbali na kuwataka kulipa bili hizo kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa.

Aidha pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha kuweza kutoa agizo hilo pia amemwagiza kamanda wa polisi mkoani hapa kuhakikisha anafanya msako kuweza kuwabaini wale wote wanaotumia umeme kinyemela na kuwafikisha katika vyombo vya kisheria.

Displaying IMG_20170429_121619.jpg
Mkuu wa Mkoa Mrisho  Gambo akishiriki kwa kuweka  tofali katika Ujenzi wa kituo cha Afya cha Moshono 
Kabla ya kutoa agizo hilo msimamizi wa udhibiti wa mapato wa shirika hilo la umeme Bi. Fatuma Boute aliweza kutoa taarifa fupi ya mradi huo ambao umegharimu kiasi cha sh.zaidi billion 128

Mh.Mrisho Mashaka Gambo amehitimisha rasmi ziara yake ya siku tano leo,kwa kutembelea kituo kikubwa cha umeme kilichopo Njiro,uzinduzi wa barabara ya Bp sunflag,kituo cha afya katika kata ya Moshono pamoja na uzinduzi wa vyumba vya madarasa.katika ziara hiyo ya siku tano pia aliweza kufanya mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi pamoja na kufahamu kero mbalimbali zinazowakabili.

No comments