Update:

Rais wa Sierra leone aahidi kukabidhi madaraka kwa amani kwa mrithi wake mwaka ujaoRais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amesema kuwa mwaka ujao ataondoka madarakani na kukabidhi madaraka kwa amani kwa mrithi wake.
Katika hotuba yake ya mwisho kuhusu hali ya nchi iliyotolewa katika maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru wa nchi hiyo, rais Koroma amesema alikuwa anaacha urithi wa amani na umoja ambao wananchi wa Sierra leone wanatakiwa kuulinda kithabiti. Amesema katika miaka 10 aliyokuwa madarakani, anaona fahari kwa mafanikio yaliyopatikana nchini humo, akiongeza kuwa Sierra Leone imepitia kipindi cha amani na utulivu wa serikali.
Sierra Leone inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwezi Machi mwaka ujao.

No comments