Update:

Okwi ana hamu ya kupata taji Ligi Kuu Uganda

Related image

Wakati Ligi Kuu Uganda ikielekea ukingoni, mshambuliaji wa SC Villa, Emmanuel Okwi amekiri wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kupata ubingwa msimu huu.Pamoja na kukiri kuwa ubingwa utakuwa mgumu kwao kwa sababu ya kutegemea matokeo ya wapinzani wao, lakini Okwi amesisitiza kwamba hawawezi kurudi nyuma kwa sababu kimahesabu jambo hilo linawezekana.
SC Villa ipo nafasi ya pili wakitofautiana kwa mabao na vinara KCCA baada ya timu hizo kutoka sare 1-1 mwishoni mwa wiki.
Akizungumza na mtandao wa Kawowo Sports, Okwi alisema walicheza vizuri na kumiliki mpira hata hivyo bahati haikuwa kwao.
Okwi alisawazishia Villa kwa bao la shuti la umbali wa mita 12 na kufuata bao la awali la KCCA lililofungwa na Geofrey Sserunkuma.
Villa sasa italazimika kuomba dua baya kwa KCCA ilipoteza mechi zake zilizosalia na wenyewe kushinda mechi zilizosalia ili kujihakikishia kutwaa ubingwa msimu huu.

No comments