Update:

Kijana wa umri wa miaka 15 auwawa kwa kupigwa Risasi na Askari wa Suma JKT Wilayani Arumeru

NA; ANNA MCHOME -ARUSHA

 
Wananchi wa kata ya lemanyata wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wamelazimika kuandamana kwa kupinga kitendo cha kupigwa risasi kwa kijana mwenye umri wa miaka 15 na askari wanaolinda katika msitu unaozunguka eneo hilo suma JKT na kudai kuchoshwa na vitendo hivyo

Wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la kupigwa risasi wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali iwasaidie na iwatendee haki na kuangalia matukio kama haya ambapo hili ni tukio la pili kutokea wilayani Arumeru

Naye kwa upande wake diwani wa kata ya lemanyata ndg Losieku Kilisu ameezea tukio hilo na kusema kijana huyo ameuwawa akiwa anapita eneo la msitu na hajatuma watu waandamane ila wanakijiji walimuuliza nan ananguvu kama wilaya ilionya na hawajatii ndipo wakaamua kuandamana mpaka kwa mkuu wa mkoa

Akizungumza na wananchi baada ya kuzuia maandamano mkuu wa wa polisi wa wilaya ya Arumeru amewaomba wananchi kutulia na kuwasikiliza na kuwaahidi watashirikia na viongozi wa kijiji katika huhakikisha usalama wa maisha na mali zao na utaratibu wa sheria utafatwa ambapo watuhumiwa tayari wameshakamatwa kufuatilia tukio hilo


Tukio hili la kupigwa risasi kwa kijana huyu limefuatia tukio la kupigwa risasi la watu watano katika kata zinazouzunguka msitu huo na kupelekea watu hao kufariki dunia huku wananchi hao wakidai kuchoshwa na vitendo hivyo ambavyo wamekuwa wakifanyiwa.

No comments