Update:

Msanii wa Zimbabwe ashirikiana na wasanii kutoka nchi nyingine ikiwemo China kutengeneza wimbo

Msanii wa kimataifa wa Zimbabwe Bw. Abraham Matuka atatoa wimbo wa ushirikiano wa kimataifa mwezi huu, wenye lengo la kuhimiza utalii wa Zimbabwe na maelewano ya kiutamaduni kati ya nchi mbalimbali.
Msanii huyu atashirikiana na wasanii sita kutoka China, Malaysia, Indonesia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Angola na India ili kutengeneza wimbo huo uitwao "Lovely Zimbabwe".
Mwaka jana Bw. Matuka alitoa wimbo unaoitwa China-Africa ambao uliwashirikisha wanamuziki wa China ukiwa njia ya kuhimiza na kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni kati ya China na Zimbabwe. Amepokea uungaji mkono kutoka jamii ya wachina wanaoishi nchini Zimbabwe katika utengenezaji wa wimbo huo.

No comments