Update:

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anaendelea na ziara yake ya siku tano ikiwa leo ni siku ya 4


 
Rc Mrisho Gambo ametembelea na kukagua ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo yenye urefu wa Km 5.9 ambayo inagharimu sh 17,979,985,486.00 hadi kukamilika kwake.

Mjenzi wa Barabara hiyo kupitia kampuni ya Jiangxi Geo Engineering (Group) Carpotation. Barabara hio ambyo itaunganisha kata za Themi,Sokon One,Unga Ltd pamoja na sinon pamoja na kuunganisha barabara za Unga Ltd na Murriet. Huku lengo kuu la mradi likiwa ni kuboresha miundo mbinu ndani ya jiji la Arusha na kukuza fursa za kiuchumi.

RC Gambo akipokea maelezo kutoka kwa mkandarasi wa Bara bara hiyo pamoja na huku Mwakilishi wa Mhandishi Mshauri ambaye ni msimamizi wa Barabara hiyo ENG EDWARD BENEDICT (KUSHOTO KWA MKUU WA MKOA MWENYE SHATI LA MISTARI MIYEMABABA KUSHUKA CHINI) kutoka kampuni ya UWP Cnsulting (T)Ltd ambae ndio anasimamia utekelezaji wa mradi huo akisikiliza kwa makiniKATIKA HATUA NYINGINE, Rc Mrisho Gambo amezindua Daraja la mto Ngarenero katika barabara ya Lolovono katika kata ya sokoni 1,ambapo ujenzi wa daraja hilo limejenhwa na mkandarasi Meero Contactors Ltd wa jijini arusha. Huku lenho la mradi likiwa ni kuboresha miundo mbinu ya sokoni 1.

Ambapo Mrisho Gambo amewataka wananchi wa maeneo hayo kulinda daraja hilo na kuto wataka watu kujenge pembezoni mwa mto huo kama sheria zinavyo sema huku wakiendelea kujali na kulinda miundo mbinu hiyo hasa daraja hilo liloghalimu kiasi cha sh 195,705,419.oo hadi kukamilika kwake

No comments