Update:

Mchungaji Getrude Lwakatare aapishwa bungeni

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amemuapisha Dkt Getrude Rwakatare kuwa Mbunge wa viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Lwakatare ameapishwa mapema Alhamisi, Mjini Dodoma na Spika Ndugai, baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Aprili 14 mwaka huu ili kujaza nafasi iliyoachwa na Sophia Simba ambaye alivuliwa uanachama wa CCM kwa madai ya uvunjifu wa maadili ya kichama.
Dkt Getrude Lwakatare anaingia katika bunge hilo kwa mara ya pili baada ya mwaka 2007, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Salome Mbatia ambaye alifariki dunia.

No comments