Update:

Mbarawa aonya wanaohujumu miundombinu ya barabara mpya

Akizungumza jana kwenye ziara yake katika mikoa ya Manyara na Arusha, alisema miundombinu ya barabara inajengwa kwa gharama kubwa, hivyo kuwahimiza wananchi kuitunza kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Alisema barabara ya Kia hadi Mirerani inayojengwa na Kampuni ya Chico, yenye urefu wa kilomita 26 kwa gharama ya Sh34 bilioni ni ya kihistoria kwa sababu tangu nchi ipate uhuru, hawakuwahi kupata barabara ya kiwango cha lami licha ya eneo hilo kuwa maarufu kwa uchimbaji wa madini ya Tanzanite.
Mkazi wa Mirerani, Rashid Bakari alisema licha ya kufurahia barabara hiyo, lakini kuna changamoto ya mitaro na njia za kuingia kwenye mitaa yao ambazo hazipitiki kutokana na mitaro iliyochimbwa na mkandarasi.
Katika ziara yake hiyo, Mbarawa alikagua barabara ya mchepuko kutoka Ngaramtoni hadi Makumira wilayani Arumeru yenye urefu wa kilomita 42.4, ambayo ujenzi wake umeanza na inajengwa chini ya mpango wa uboreshaji miundombinu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Simanjiro. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewataka wananchi kutohujumu miundombinu ya barabara mpya iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) hadi mji wa Mirerani wilayani Simanjiro.
Profesa Mbarawa pia, alikagua ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 14.1 yenye njia nne kutoka Sakina hadi Tengeru wilayani Arumeru zinazojengwa na Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture LTD, kwa gharama ya Sh139 bilioni inayotarajiwa kukabidhiwa mwezi ujao.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Arusha, Mhandisi Mgeni Mwanga alisema kumekuwapo na changamoto za barabara hiyo kukamilika kwa wakati kwa sababu ipo mjini, eneo lenye msongamano wa magari.
Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho ujenzi unakaribia kukamilika na kwamba, njia zote muhimu za kuingia barabara kuu zitawekwa katika mazingira ya kupitika. 

No comments