Update:

Mauricio Pochettino awashushua wanaowanyemelea wachezaji wa Tottenham hotspurs


Meneja wa klabu ya Tottenham hotspurs, Mauricio Pochettino, amesema, klabu yake kamwe haitauza wachezaji wake tegemezi katika kipindi hiki cha majira ya Joto na badala yake watakaouzwa ni wale watakaoonekana hawana umuhimu ndani ya klabu hiyo.Kikosi hicho kinachoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza nyuma ya klabu ya Chelsea kinaahidi kulinda wachezaji wake wasije wakachukuliwa na klabu nyingine zilizoanza kunyemelea katika kikosi hicho. Pochettino amesema kua ana mahusiano mazuri na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy ambae amemuhakikishia klabu hiyo haitauza wachezaji wake na kamwe haina haja na fedha, na kuongeza, wachezaji wao watasalia ndani ya klabu.
Beki wa kikosi hicho, Kyle Walker na Danny Rose pamoja na viungo wa kati Christian Eriksen na Dele Alli ni miongoni mwa wachezaji wanaosemekana kukikacha kikosi hicho cha White Hart Lane, suala ambalo linaumiza vichwa uongozi wa klabu hiyo.
Meneja huyo amesema, anaona kuwa wanafanya vizuri ndio sababu klabu nyingi zenye uwezo zinawatolea macho wachezaji wao wenye vipaji vikubwa.

No comments