Update:

Man United na Man City hakuna mbabe


Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 iliendelea jana usiku kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Etihad jijini Manchester.
Mchezo huo ulizikutanisha timu mahasimu kutoka jiji la Manchester kati ya Man United waliowafuata Man City katika uwanja wao wa Etihad kucheza mchezo wao wa 33 wa Ligi Kuu England ambao walilazimishana sare ya bila kufungana.
Mvuto na upinzani wa Manchester Derby umeongezeka kutokana na upinzani wa kocha Jose Mourinho wa Man United na kocha Pep Guardiola wa Man City ambao walitoka nao toka LaLiga mmoja akiwa anaifundisha Barcelona na Mourinho akiifundisha Real Madrid.
Man city wakiwa wenyeji wa mchezo huo waliutawala mchezo kwa asilimia kubwa na umiliki wa mpira ukiwa ni asilimia 69 kwa 31.
United walibaki pungufu katika dakika ya 84 baada ya kiungo wake Marouane Fellaini kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu, baada ya kumpiga kichwa Sergio Aguero. Huu ulikua ni mchezo wa 24 kwa Man united wakicheza bila kupoteza msimu huu.

No comments