Update:

Mahakama kutoendelea na shauri la Kesi ya kughushi nyaraka na kujifanya Afisa usalama wa Taifa inayo mkabili Lengai Ole Sabaya


Image result for lengai ole sabaya
Na Anna Mchome ; Arusha
Kesi ya kughushi nyaraka na kujifanya Afisa usalama wa Taifa,inayomkabili mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Arusha,Lengai Ole Sabaya imeshindwa kuendelea Mara baada ya upande wa Mashtaka kudai haina nia ya kuendelea na shauri hilo.
Akizungumza mahakamani hapo mbele ya hakimu Gwanta Mwankuga,Wakili wa serikali Grace Madikenya alisema kuwa jamhuri kupitia kifungu namba 91 cha mwenendo wa makosa ya jinai haina nia na shauri hilo kutokana na shahidi wake muhimu kwenda masomoni nje ya nchi.
"Mheshimiwa hakimu upande wa jamhuri haina nia ya kuendelea na shauri hilo chini ya kifungu namba 91 cha mwenendo wa makosa ya jinai"Alisema wakili wa serikali
Hata hivyo Wakili wa upande wa mshitakiwa,Grace Mndeme na Charles Abrahamu  waliweka pingamizi juu ya hoja hiyo walidai kuwa Wakili wa serikali wanania ya kuichezea mahakama na wanalengo la kumtesa mteja wao.
" Mheshimiwa sisi tunapinga hoja iliyoletwa mbele yako na Wakili msomi wa serikali kwa sababu upande wa jamhuri wanaitumia vibaya mahakama na wanania ya kumtesa mshitakiwa,na si Mara yao ya kwanza kufanya hivyo"Alisema Mndeme
Alieleza kuwa hoja ya wakili wa serikali haina nia njema na mshitakiwa kwani sio Mara ya kwanza kueleza nia ya kutoendelea na shauri hilo na baadae  mtuhumiwa anapoachiwa hukamatwa na kulazwa mahabusu na baadae kufikishwa mahakama na kushitakiwa kwa shauri hilo hilo.
Pia aliieleza mahakama hiyo kuwa kumekuwepo na uzembe katika uendeshaji wa shauri hilo unaofanywa na Mwanasheria wa serikali ,kwa sababu wakati kesi hiyo inaendelea walishindwa kuleta mashahidi badala yake walikimbilia kuliondoa shauri hilo mahakamani.
Baada ya kuwepo kwa pingamizi hilo kutoka kwa mawakili wa mshitakiwa ,hakimu Mwankuga aliahirisha shauri hilo kwa Madai kuwa atatoa uamuzi Mdogo siku ya Ijumaa ,Mai 28 mwaka huu.
Akizungumza nje ya mahakama mshitakiwa, Sabaya alieleza kukerwa na hatua ya upande wa serikali kuendelea kupiga danadana kesi yake alidai kuwa kuna mpango wa kuendelea kumdhalilisha kwani yeye ni mwanasiasa aliyechaguliwa na wananchi anahitaji kuwatumikia .

No comments