Update:

Maamuzi ya Mahakama Arusha kuhusu kesi ya aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM

  
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo April 28, 2017 imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, Lengai Ole Sabaya ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kughushi na kutumia kitambulisho cha Usalama wa Taifa.

Hakimu Gwanta Mwankuga ambaye alikuwa anasikiliza kesi hiyo, amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kupeleka mashahidi katika kesi hiyo na kusema Mahakama haijamuachia huru mshtakiwa kwa ombi la Jamhuri kutaka kuondoa shitaka hilo Mahakamani, bali amemuachia kwa kifungu cha sheria namba 225 kipengele cha 5.

No comments