Update:

KRC Genk na AS Eupen zatoshana nguvu Ligi ya Ubelgiji

Image result for KRC Genk vs AS Eupen

Michezo ya mtoano ya Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2016/2017 imeendelea tena jana kwa michezo minne kuchezwa, KRC Genk anayoichezea mtanzania Mbwana Samatta ilikuwa ugenini kucheza mchezo wao wa 5 wa mtoano wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya wenyeji wao AS Eupen.

KRC Genk waliingia uwanjani kucheza mchezo huo wakiwa wana rekodi ya kuwa timu pekee katika timu 12 zinazocheza mechi hizo kutofungwa mchezo hata mmoja wakiwa wameshinda michezo yote minne, hata hivyo jana wakiwa ugenini wamelazimishwa sare ya 1-1 na kuwafanya kupata sare ya kwanza.

AS Eupen licha ya kuwa nyumbani walianza kufungwa goli dakika ya 20 mchezaji Malinovsky akipachika goli la kwanza la Genk lakini AS Eupen walisawazisha goli hilo dakika ya 51, katika michezo ya mtoano KRC Genk na AS Eupen ndio timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo katika timu 12 za Kundi A&B lakini AS Eupen wameshinda mechi moja pekee kati ya tano.

No comments