Update:

Kocha Antonio Conte akiri michezo miwili ya siku za hivi karibuni ni migumu kwa upande wao


Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, amekiri michezo miwili waliyocheza siku za hivi karibuni imekua michezo migumu kwa upande wao na imekua muhimu kuhakikisha wanapata alama tatu zitakazowasaidia kujikuta kileleni mwa ligi hiyo ya EPL. Conte ambaye ni raia wa Italia, amewasifia wachezaji wake kwa kupambana hadi kuhakikisha wanachomoza na ushindi Mnono wa magoli 4 kwa 2 mbele ya kikosi cha Southampton, na anaamini kuwa wachezaji wake watapambana na kuhakikisha wana nyakua Ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza kwa Msimu huu. Meneja huyo mwenye Mizuka pindi timu yake inapopata ushindi, amesema kuwa anahitaji kukipumzisha kikosi chake baada ya Michezo hiyo migumu waliyokutana nayo wiki hii.
The Blues wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na alama 78 wakiwa wamecheza michezo 33 huku Tottenham ikiwa katika nafasi ya pili kwa alama 71 wakiwa nyuma ya Chelsea kwa mchezo mmoja.
Majogoo wa London, klabu ya Liverpool, inashikilia nafasi ya 3 wakiwa na alama zao 66 huku matajiri wa Uingereza Manchester City, wakishikilia nafasi ya 4 wakiwa na alama zao 64 nyuma ya klabu ya Mashetani wekundu Manchester United inayoshikilia nafasi ya 5 na alama zao 63 wakiwa nyuma kwa alama 1 dhidi ya City.

No comments