Update:

BENDERA CUP KUANZA RASMI APRIL 29 2017 MKOANI MANYARA


Na Clement Shari Image result for Joel Bendera


Mashindano ya mpira wa miguu yaliyopewa jina la mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera maarufu kama Bendera Cup yaliyokuwa yaanze kutimua vumbi kuanzia April 22 ya mwaka huu katika uwanja wa Qwaraa wilayani Babati sasa yataanza rasmi tarehe 29 April.

Sababu ya mashindano hayo kusogezwa mbele ni kutokana na maandalizi ya uwanja wa Qwaraa Babati kutokukamilika kwa wakati ikiwa ni pamoja na uzio wa uwanja huo.

Mmoja ya waratibu wa mashindano hayo Bwana Haile Baa Mukusi ameiambia Blog ya M- Media Tz  kuwa maandalizi yote kuelekea michuano hiyo yanaendelea vizuri na hadi hivi sasa jumla ya vilabu 16 vimethibitisha kushiriki katika mashindano hayo na tayari vimekwishalipa ada ya ushiriki ambayo ni shilingi elfu 40.

No comments