Update:

Bella Fasta awawashia moto wasanii wa filamu alioandamana kisa filamu za...

Msanii wa muziki na filamu, Bella Fasta amefunguka kwa kudai kuwa
hajapendezwa na kitendo cha baadhi ya wasanii wa filamu nchini
kuandamana kupinga filamu za nje, kwa madai hatua hiyo ilitakiwa
kujadiliwa na wasanii wote wa filamu na siyo vikundi vya watu fulani
ndani ya tasnia hiyo.

Wasanii hao ambao waliandamana wakiongozwa na Jacob Stephan ‘JB’,
waliiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kupiga marufuku
wafanyabiashara wa filamu za nje kwa madai hawalipi kodi wakati wasanii
wa ndani wanalipa 30% ya mapato ya filamu zao.

 Bella amedai tukio hilo lilitakiwa kuwa na kauli moja ya wasanii wote wa filamu.
“Bongo Movie mmeniudhi, sana siyo wote, ni wachache,” alisema Bella
Fasta kwa ukali na kuongeza “Yaani hamuoni aibu mnasema kabisa movie za
nje zisiingie Tanzania, nchi gani mambo haya yapo?. Tufanye kazi nzuri
ziuze siyo tunaingiza mambo ya siasa kwenye mambo yetu ya kawaida,”


Bella amesema, kama ilikuwa ni ajenda ya wasanii wote kuhusu kuibiwa kazi zao mbona wasanii wa muziki hawakuhusishwa.

“Kama hilo suala lingekuwa ni letu sote yanii wasanii wote
tungeungana Bongo Movie wote au na wasanii wa muziki kwanini hawapo? au
kuna kitu,” alisema Bella.

Steve Nyerere ni kati ya wasanii wa filamu ambao wamepinga harakati hizo.
SOURCE: BONGO 5

No comments