Update:

Bei za vyakula nchini juu

Bei za vyakula  katika baadhi ya masoko nchini zimepanda na kusababisha hali ya maisha kuwa ngumu.
Uchunguzi uliofanywa kwenye baadhi ya masoko jana na juzi umebaini kuwa bidhaa mbalimbali zimepanda bei yakiwamo maharage ambayo yamepanda kutoka Sh 1800 hadi 2700 na 3000 kwa kilo.
Pia Sukari imepanda kutoka bei elekezi iliyotolewa na Serikali ya Sh1800 hadi Sh 2500, Mchele kutoka Sh 1200 hadi 2600 kwa kilo.
Unga wa sembe nao umepanda kutoka Sh1200 hadi Sh 2000. Bidhaa nyingine zilizopanda ni mboga za majani ambapo fungu la mchicha, chainizi, tembele limepanda kutoka Sh200 hadi Sh400 na Sh 500.
Nyanya ambazo mwaka jana, ziliuzwa kwa bei nafuu hadi kufikia Sh 1500 kwa sadolini, msimu huu zimepanda ambapo nyanya moja inauzwa kwa Sh 200 hadi 300 kutoka Sh200 nyanya tatu au nne.
Akizungumzia bei za vyakula kupanda, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage amesema suala hilo liko kisayansi linalohitaji taarifa sahihi na hivyo asingeweza kutoa majibu bila kukusanya taarifa hizo.

No comments