Update:

Arusha:Watuhumiwa wa Ugaidi wagoma kupandishwa kizimbani wakidai mpaka upelelezi utakapo kamilika

NA MICHAEL NANYARO
Mahakama kuu kanda ya Arusha imelazimika kuahirisha kesi ya ugaidi inayowakabili jumla ya watu 61 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika leo mahakamani hapo kufuatia watuhumiwa hao na kugoma kufika mahakamani,kwa madai kuwa wamechoka kupigwa tarehe na wanataka kesi yao ifanyiwe upelelezi pindi upelelezi huo utakapo kamilika nao  wataweza kufika mahakamani.

Katika kesi hiyo ambayo inawakabili jumla ya watu 61 kwa tuhuma za ugaidi waliweza kufika watuhumiwa tisa miongoni mwao mwanamke akiwa mmoja  kati ya idadi ya watuhumiwa hao ambapo kwa mujibu wa hakimu mkazi wa mahakama hiyo hakimu Gwantwa Mwankuga ameeleza mahakamani hapo kuwa walipokea taarifa kutoka magereza kuu Kisongo kuwa baadhi ya watuhumiwa waligoma kwenda mahakamani wakidai kuchoshwa na kupigwa tarehe za shauri lao.

Shauri hilo amablo limeahirishwa leo mahakamani hapo limepangwa kufanyika tena aprili 25 mwaka huu ambapo watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la ugaidi na kujikuta wakikaa mahabusu kwa kipindi cha miaka minne hadi hivi sasa huku shauri lao likiwa linaendelea mahakamani.

No comments