Update:

Arusha:Watuhumiwa kesi ya ugaidi wagoma kushuka kwenye Gari la magereza

Picha na Michael NanyaroMahakama ya hakimu mkazi Arusha Jana wamesikiliza shauri la watuhumiwa 61 wa makosa ya ugaidi chini ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Nestory Baro Na mwendesha mashtaka wa serikali Grace Madikenya.
Picha na Michael Nanyaro

Watuhumiwa hao walifikishwa kwenye viwanja vya mahakamani hapo Majira ya saa 9:27 na gari la magereza lenye mamba MT0040 tukio lililo ambatana na baadhi ya mahabusu 29 kugoma kushuka kwenye basi na wengine 32 kuitikia agizo la mahama la kwenda kusikiliza mashauri yao .
Picha na Michael Nanyaro

Tukio hilo la kugoma kwa watuhumiwa hao kushuka kwenye basi kumepelekea kusimama kwa shughuli za mahakama kwa zaidi ya saa moja ili kutafuta njia sahihi ya kutatua tatizo hilo.

Wakizungumza mahakamani hapo watuhumiwa 32 waliopanda kizimbani walisema kuwa wamehamua kuitikia agizo la mahakama kutokana na barua iliyotoka kwa mkuu wa upelelezi wa Mkoa (RCO) kuwa Madai yao yamefanyiwa kazi ambapo aliwataka kusitisha mgomo.

"Tumekuja mahakamani kusikiliza nini walichotuitia ili tujue wapi mahakama walipofikia kwenye upelelezi wao laki cha kusikitisha mambo ni Yale Yale ya kupigwa tarehe kutokana na hali hiyo hatutakuja tena maana tumecho kuzungushwa"

Wameitaka mahakama kuwaacha mahabusu mpaka upelelezi wao utakapo kamilika kwa sababu shauri lao lina muda mrefu tangu mwaka 2014 bila kufanyiwa kazi.

Walitaka kujua mashauri yao ni namna gani yamefanyiwa kazi ili kujua kesi yao ilipofikia na hakimu atakayesikili

"Tupo tayari kufungwa kama kweli tunamakosa tunasikitishwa na upande wa upelelezi kushindwa kufanya kazi yake kwa wakati kama wameshindwa kupata ushaidi wa kuthibitisha tuhuma hizo basi waachiwe huru

Walisema mgomo huo utaendelea mpaka upande wa jamuhuri utakapokuwa tayari kuwasomea mashtaka au kuwaachia huru.

Akijibu Madai hayo hakimu mkazi wa mahakama hiyo Nestory Baro alisema kuwa mkuu wa kitengo cha upelelezi Mkoani hapa umeshakamilisha uchinguzi wao na majalada wamepeleka makao makuu ambapo amehairisha shauri hilo adi mei 8 mwaka huu. Mwisho

No comments