Update:

8 wafariki kwa ajali ya ndege ya jeshi Cuba


Wanajeshi 8 wafariki kufuatia ajali ya ndege Magharibi mwa Cuba

8 wafariki kwa ajali ya ndege ya jeshi Cuba
Ndege ya kijeshi imeripotiwa kuanguka katika eneo la milima la wilaya ya  Artemisa maghariba mwa Cuba na kupelekea vifo vya wanajeshi 8.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya tukio hilo ni kuwa ndege hiyo aina ya AN-26 ilianza safari siku ya Jumamosi majira ya asubuhi kutoka uwanja wa ndege wa Playa Baracoa na kuanguka katika eneo la milima la mji wa Candelaria.

Jeshi imefahamisha kwamba timu maalum ya wataalamu wa uchunguzi itafanya utafiti kuhusu ajali hiyo ingawaje hawakutoa taarifa zaidi.

No comments