Update:

Zoezi la ujenzi wa barabara linaendelea kwa kiwango changarawe Jijini Arusha

Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kupitia Idara ya Ujenzi bado ipo katika ukarabati wa barabara zake ndani ya halmashauri kuhakikisha miundo mbinu ya barabara zote ndani ya Halmashauri zinapitika kwa kipindi cha mwaka mzima.
Shughuli za ukarabati wa barabara ya Ngaramtoni - Selian Loning'o mpaka Ilboru yenye urefu wa Kilomita tisa (9) ambayo itawahudumia wananchi wa maeneo hayo na vitongoji vyake.
Halmashauri inafanya ukarabati wa kawaida kwa kiwango cha  changarawe (Moram) katika barabara hiyo.
Halmashauri kupitia idara ya ujenzi imetoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kuwa waendelee kutambua kuwa barabara hizo ni mali yao na  ndio wamiliki wa barabara hizo,  hivyo wametakiwa  kuzitunza barabara hizo kwa kutokufanya uharibifu wa aina yoyote, kufanya shughuli za kibinadamu ndani wala pembezoni mwa barabara, pasiweke matuta yasiyo rasmia katika barabara, msipitishe mifugo kwenye barabara hizo, msitupe takataka wala kuelekeza mifereji ya maji machafu barabarani! kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Barabara ni yetu kwa pamoja tuzitunze