Update:

01 March 2017

Watu 3 wakamatwa kwa uvuvi haramu MwanzaWatu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani nyamagana mkoani Mwanza kwa tuhuma za kukutwa na kilo mia tano za samaki wachanga aina ya sangara ambao hawaruhusiwi kuvuliwa kisheria.

Kamanda wa polisi wa mkoa Mwanza Ahmed Msangi ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na uvuvi haramu maeneo ya maziwa na baharini na kusema kuwa jeshi limejipanga kukabiliana nao.

Kamanda Msangi amesema jeshi la polisi limejizatiti kukabiliana na ongezeko la vitendo uvuvi wa kutumia zana haramu katika ziwa Victoria ambavyo tayari vimeathiri ustawi wa jamii.

Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
credit:tbc