Update:

Wananchi wa Loliondo wazuia msafara

Msafara wa Kamati ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii iliyokuwa ikitembelea Pori Tengefu la LOLIONDO Wilayani NGORONGORO umezuiliwa kwa muda na Wananchi wakishinikiza kutatuliwa kero zao.

Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya mkutano kati ya wakazi wa Kijiji cha MBUKENI na Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na utalii wakati kamati husika ikijaribu kumaliza mgogoro uliondumu kwa miaka mingi.

 Kamati hiyo imekutana na kundi la wakazi wa maeneo jirani maarufu kama wafugaji katika Kijiji cha MBUKENI.
       
Baadhi ya wajumbe wa kamati wamesema hatua ya kuzuia msafara inalenga kuzuia kukwamisha juhudi za usuluhishi.
       
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa JUMANNE MAGHEMBE amesema hifadhi ya eneo hilo lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 1500 ina umuhimu mkubwa.