Update:

Waliokaidi sensa ya makazi waathirika na mgao wa ruzuku

Serikali imesema baadhi ya maeneo nchini yanapata mgawo mdogo wa Fedha za ruzuku na huduma mbalimbali za Kijamii kutokana na kukaidi Kushiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambalo msingi wake ulikuwa kuweka Mipango ya kuhudumia vyema wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Selemani Jafo wakati akizungumza na watumishi Wilayani Liwale Mkoani  Lindi

Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa na ukaidi wa kufuata maagizo ya serikali ambayo msingi wake Mkubwa ni kutaka kuweka Mipango bora ya Kutoa huduma lakini kwa Jeuri tu baadhi ya watu wakikaidi maagizo ya serikali

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale  amesema Halmashauri hiyo inashindwa kuendesha shughuli zake kutokana na kutopelekewa fedha za kutosha za ruzuku.

No comments