Update:

03 March 2017

Vanessa Mdee adai kuna wasichana walichukia alichoimba kwenye Dume Suruali

Akiongea kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir Alhamis hii, Vanessa amedai kuwa kuna wasichana kibao waliokerwa na alichokiimba kwenye wimbo huo.
“A lot of women were offended with Dume Suruali,” alisema.
“Huwezi kuamini kuna akinadada wengi sana waliniambia ‘kwahiyo wewe Vanessa unatuambia nini.’ And you know sehemu yetu kwenye jamii kama wasanii ni kuigiza japo hata sometimes kama haufanyi kile kitu, you are supposed to tell the story of the people of the society. So hiyo ndio ilikuwa nafasi yangu kwenye Dume Suruali, nilikuwa nahadithia tu. So I hope they are not offended,” aliongeza.
Hata hivyo Vanessa amedai kuwa kufanya kazi na Mwana FA kwenye wimbo huo ilikuwa ni baraka kubwa na ni kitu alichokuwa akikiota kwa muda mrefu.
source:bongo5