Update:

Umoja wa Afrika washtushwa na mashambulizi dhidi ya wanafunzi wa Kiafrika nchini India

Umoja wa Afrika umesema umeshtushwa vikali na mashambulizi dhidi ya wanafunzi wa Kiafrika katika mkoa wa Noida na mikoa mingine nchini India.
Umoja huo umelaani vurugu zilizotokea wakati wa maandamano yaliyoanza jumatatu yakiwalenga Waafrika kutoka nchi mbalimbali, hususan Nigeria, ambazo zilisababisha kupoteza maisha kwa watu wasio na hatia pamoja na majeraha.
Taarifa ya Umoja huo pia imesema, mashambulizi hayo pia yamesababisha Waafrika wengi kukimbia makazi yao ya kawaida, na hivyo kuhatarisha zaidi maisha yao.
Umoja wa Afrika umezitaka mamlaka nchini India kutoa msaada unaotakiwa katika kuwatibu majeruhi wa mashambulizi hayo.

No comments