Update:

Ummy Mwalimu: Sheria ya ndoa lazima irekebishwe

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ni lazima ifanyiwe marekebisho ili kulinda haki za watoto nchini.
Akizungumza leo (Alhamisi) wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kitaifa inayohusu ndoa za utotoni, Mwalimu amesema ndoa za utotoni ni kikwazo kwa maendeleo ya Taifa hasa kwa wanawake. Utafiti huo uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Idai ya Watu(UNFPA), CDF, Repoa na Plan International kwa kushirikiana na Wizara ya Afya umejikita kuangalia visababishi vya ndoa za utotoni ambapo mojawapo ni umasikini, mila potofu na sheria zisizo rafiki.
"Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ni kichocheo cha kuwafanya watoto wapate mimba.Ipo haja ya kufanya marekebisho,"amesema Mwalimu.

No comments