Update:

Serikali kuwaondoa wahamiaji haramu MkingaWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba amesema Serikali itafanya operesheni maalum ya kuwaondoa wahamiaji haramu ambao wanachangia uharibifu wa mazingira katika Wilaya ya Mkinga.

Makamba alitoa kauli hiyo leo baada ya kupokea taarifa ya kuwapo kwa wahamiaji hao kutoka nchi jirani ya Kenya na kusema Serikali haitowavulimia watu wanaoharibu mazingira ya nchi.

Amesema kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na wahamiaji hao ni lazima Serikali ichukue hatua madhubuti ili kuukomesha. Makamba ambae pia ni Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, amesema uharibifu unaofanywa na wahamiaji hao wakukata miti na kichoma mkaa ni jambo ambalo limemuumiza kama Waziri mwenye dhamana na mazingira.

No comments