Update:

Paa la Maabara lajeruhi wanafunzi ROMBOWanafunzi SABA kati ya 14 wa Shule ya Sekondari ya MRAMBA iliyoko wilayani ROMBO mkoani Kilimanjaro wamelazwa katika hospitali ya HURUMA wakipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na paa la maabara kufuatia upepo mkali iliyoambatana na mvua na kuezua paa la maabara hiyo.Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Shule ya sekondari ya MRAMBA, FLAVINA USINGA amesema maabara hiyo ilikuwa bado katika ujenzi licha ya kuwa wanafunzi walikuwa wakifanya mazoezi yao kwa masomo ya sayansi.USINGA amesema wakati mvua iikiendelea kunyesha wanafunzi hao walisimama nje ya maabara hiyo kujikinga na mvua ndipo paa la maabara likaezuliwa na kusababisha maafa ikiwemo wanafunzi kujeruhiwa vibaya.Akiwa katika hospitali ya HURUMA alipowatembelea wanafunzi hao kuwajulia hali, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro SAID MECK SADICK amemuagiza Mkuu wa wilaya hiyo AGNESS HOKORORO kukaa pamoja na kamati ya maafa ili kuhakikisha wanezeka jengo hilo liendelee kutumika.

No comments