Update:

Nay apewa mualiko na JPM Ijumaa hii Ikulu

Saa chache baada ya kuachiwa huru na Jeshi la Polisi Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego apata mualiko wa kwenda  Ikulu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli.
Nay amepata mwaliko huo baada ya kauli ya raisi Magufuli kuamuru kuachiwa huru na jeshi la polisi lililomshikilia  tangu Jumapili na wimbo wake uliokuwa umefungiwa kufunguliwa rasmi  kuendelea kuchezwa na kusambazwa.
Msanii Nay  alikiri kupata mwaliko huo jana na kusema kuwa ameambiwa aende siku ya Ijumaa ili kufanya mazungumzo na Rais.
“Yeah ni kweli jana nilipa mwaliko lakini nimeambiwa niende Ijumaa kwa sababu kuna ugeni unakuja kwahiyo na mimi nimealikwa kuhudhuria,” alisema Nay.
Nay alikamatwa na polisi Jumapili iliyopita mkoani Morogoro na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kutunga wimbo wenye maudhui yanayoikashifu Serikali.
Mapema jana mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe ambae alikua umeupiga stop wambo wa WAPO wa msanii huyo, alisema Rais Magufuli ameagiza msanii huyo aachiwe huru na wimbo wake uendelee kuchezwa na kusambazwa.

No comments