Update:

Nape aomba TCRA isichukue hatua kwa vyombo vya habari

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutovichukulia hatua vyombo vya habari mara kwa mara na badala yake vinapokosea wavirejeshe katika mstari sahihi kwa upendo.
Nape ametoa ombi hilo leo wakati wa uzinduzi wa matangazo ya kituo cha redio cha EFM katika mikoa mipya 10 na kusema kwa kuwa vyombo vya habari nchini ni mhimu na vina nia njema kwa Taifa vinapokosea vinatakiwa kurekebishwa na kutiwa moyo. "TCRA nawaomba mambo mengine msifumbie mamcho yote fungeni jicho moja ili mambo yaende mbele.
Mnalo jukumu la kivilea vyombo vya habari na ni kawaida mtoto anayekuwa kuanguka na kujikwaa hivyo wakati mwingine muwaonyee tu sio kuwachapa kila wakati," amesema Nape

No comments