Update:

16 March 2017

Namuunga mkono Makonda kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya – Cyrill Kamikaze

Hitmaker wa ‘Shori’ anayefanya poa kwa sasa na ngoma yake mpya ‘Sinunui Stress’ Cyril Kamikaze ni mingoni kati ya wasanii wanaomuunga mkono mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika mapambano yake dhidi ya biashara na utumiaji wa dawa za kulevya.
Kupitia wimbo wake mpya Kamikaze amesema “vipi kwenye list ye habebi?, maana tushasikiaga siaga naye begi.”
Akiongea kwenye kipindi cha Zero Planet cha Ice Fm kinachoongozwa na Gami Dee, amesema, “harakati zake kiukweli naziunga mkono, tunajua jinsi gani watu wameefektiwa na suala zima la madawa ya kulevya, wamepoteza kabisa malengo yao, halafu ukiwa addicted kuacha ni ngumu kwahiyo ndoto zao zimeshakufa, mi naunga mkono.”
Alipoulizwa juu ya safari zake za nje ya nchi mara kwa mara huwa zinahusisha kitu gani zaidi hali hatuoni kama ni show au nini kinachompeleka nje ya nchi, rapper huyo amesema, “mbali na muziki mi ni mfanyabiashara au sio? Kwahiyo kusafiri kwangu mara nyingi inakuaga biashara na wakati mwingine naenda kupumzika.”
Mbali na hayo Cyril amewataka vijana kukataa kununua stress ili kufanikisha malengo kwa kukabiliana na changamoto zilizopo mbele yako.