Update:

Mzazi aomba msaada wakusaidia mtoto wakeMkazi mmoja wa manispaa ya Singida, Zaria Hamza amewaomba wataalam na raia wema kumsaidia kwa hali na mali mtoto wake aliyejifungua mwezi uliopita akiwa hana mikono wala miguu.Amesema ingawa kwa sasa anamudu kutunza na kufanya shughuli ndogo ndogo anapatwa na hofu siku za baadae ambapo atalazimika kutumia muda wote kumtunza mtoto huyo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kukaa wala kufanya chochote kutokana na kukosa viungo hivyo muhimu.ZARIA amesema anachohitaji ni msaada wa aina yoyote ikiwa ni pamoja na ushauri wa kitaalamu wa kumsaidia mtoto huyo, huku akisikitishwa na tabia ya baadhi ya wasichana wanaotupa watoto mara baada ya kujifungua.

No comments