Update:

16 March 2017

Mrembo Nargis Mohammed aingia kwenye biashara ya urembo kupitia mtandao

Mshiriki wa zamani wa Miss Tanzania, Nargis Mohamed ameingia kwenye biashara mpya ya urembo kupitia mtandao.
Akiwa na Nafue Nyange anayefahamika zaidi Kama GlamMadam wameamua kuandaa mafunzo maalum katika fani ya urembo kwaajili ya wanawake na vijana ambao wangependa kujifunza fani hii ya urembo.
“Mafunzo hayo hayachagui jinsia, nia yeti kubwa sisi ni kuwawezesha wenzetu kwa kuwapa ujuzi ili waweze kujiinua kiuchumi kama wajasiliamali na kujijenga kimaisha sambamba na mpango wa serikali yetu kujenga ajira na kujikwamua kutoka kwenye umaskini,” alisema Nargis Mohamed.
Mafunzo hayo yanapatikana kwa bei nafuu kabisa kupitia tovuti yao www.glammadamlive.com, na wataosajiliwa wataweza kufanya malipo kupitia Vodacom M-pesa na Tigo Pesa. Kwa wale walio nje ya nchi wanaweza kutumia kadi tofauti kama VISA,MasterCard,American Express na Kadhalika.
Gharama ni shillingi elfu 10 tu za kitanzania kwa mwezi. Wasajili watahitaji simu au tablet ya aina yeyote kama iPad,Samsung na kadhalika. Tujiwezeshe na tujiinue kwa fani hii ya urembo na ujuzi huu,pamoja watanzania tunaweza.