Update:

Mjane aliyelalamika kwa JPM aburuzwa kortiniMjane Swabaha Mohamed Shisi aliyedai kutaka kudhulumiwa na Polisi, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mahakama, mbele ya Rais John Magufuli sasa kibao kimemgeukia.

Mwanamama huyo ambaye Siku ya maadhimisho ya Sheria nchini, alijitambulisha kwa Rais Magufuli kuwa ni mjane kutoka mkoani Tanga alidai hali hiyo inachochewa na mmoja wa watoto wa marehemu Shosi, aliyemtaja kwa jina la Saburia Shosi kuwa ndiye anayepanga mipango ya yeye kudhulumiwa na huku akimtuhumu kuhusika na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kutokana na tuhuma hizo dhidi yake, Saburia amemburuza mahakamani mama huyo kwa kesi ya kashfa kwa kumhusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Katika kesi hiyo namba 38 ya mwaka 2017, Saburia ambaye anawakilishwa na Wakili Abdon Rwegasira, anaiomba mahakama itamke kuwa tuhuma hizo zilizotolewa na mama huyo dhidi yake ni kashfa.

Pia, anaiomba mahakama imuamuru mdaiwa amuombe radhi na amlipe jumla ya Sh400 milioni kama fidia ya madhara aliyoyapata kwa kashfa hizo, riba pamoja na gharama za kesi.

Source:mwananchi

No comments