Update:

Mechi kati ya Ivory Coast na Senegal yasimamishwa kwa vurugu za mashabiki

Mechi ya kirafiki kati ya Ivory Coast na Senegal ililazimika kusimamishwa wakati mashabiki walipoingia uwanjani mjini Paris. Timu hizo kutoka Afrika zilikuwa na sare ya bao moja kwa moja dakika ya 88, wakati mashabiki wachache walipoingia uwanjani huku mmoja akionekana kumrukia mchezaji wa Senegal Lamine Gassama.

Wachezaji walitoka uwanjani na refa Tony Chapron akaamua kusimamisha mechi hiyo. Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane aliipatia Senegal bao la kwanza mnamo kipindi cha pili, lakini Bi Gohi Cyriac akasawazisha dakika tatu baaadaye.
Hii ni mara ya pili ndani ya miaka mitano mechi kati ya nchi hizo kusimamishwa kutokana na vurugu za mashabiki.

No comments