Update:

Mdogo wa Mchungaji GWAJIMA amshukia kaka yake

Methusela Gwajima, Mdogo wa Mchungaji Gwajima , Mkazi wa DSM na Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi- CCM amewataka watanzania kupuuza tuhuma zinazotolewa na Mchungaji Josephat Gwajima dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM POUL MAKONDA.

Gwajima amesema kazi anayoifanya Makonda katika vita dhidi ya Dawa za kulevya ni kubwa na yenye tija  kwa Taifa asitishike na tuhuma za Gwajima.

Pia ameshangazwa na kaka yake Mchungaji Gwajima kuhubiri shughuli za siasa ndani ya kanisa.

Katika hatua nyingine  Gwajima amempongeza Rais Dkt John Magufuli kutaka vita ya dawa za kulevya iendelee na kuwataka wanaccm wote na wananchi kwa ujumla kuunga mkono vita dhidi ya dawa  za kulevya.
Source:tbc

No comments