Update:

Madereva wa magereza waonywa, watakiwa kujiepusha na wizi


Askari magereza waliomaliza mafunzo ya kazi ya udereva
wameonywa kujiepusha na wizi wa mafuta, matairi na vipuri vya magari ya
jeshi hilo.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk Juma Malewa
wakati akifunga mafunzo ya madereva kozi namba 21 ya mwaka 2017 kwa
askari magereza wa kikosi cha uhamiaji yaliyomalizika katika Chuo cha
Ufundi cha KPF mkoani hapa kinachomilikiwa na jeshi hilo.

Dk Malewa alisema jeshi hilo linatarajia kupata magari takriban 900 na
kwamba kwa kuanzia watapokea magari 400, ambayo askari hao watapewa
kuyaendesha.

Mkuu wa chuo hicho, Osmund Ndunguru alisema mafunzo hayo
yaliwashirikisha wanafunzi 93 kutoka magereza

No comments