Update:

LIGI YA MKOA WA ARUSHA YAANZA KESHO

KITIMUTIMU cha Ligi ya Taifa ngazi ya mkoa wa Arusha hatua ya Sita Bora kinatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumanne ya kesho Machi 21.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Chama Soka Arusha (ARFA) timu zinazoshiriki hatua hiyo ya ligi hiyo ni pamoja na Domingo, Hobby, Arusha Meat, Nyota, Boda Boda na Future Stars.
Utepe wa ligi hiyo utakatwa kwa mchezo kati ya Domingo na Hobby Machi 21 na Machi 22 itakuwa ni kati ya Arusha Meat na Nyota Academy.

Ligi hiyo inatarajiwa kufikia tamati Machi 30 ya mwaka huu kwa mchezo kati ya Boda Boda na Arusha Meat. Bingwa wa ligi hiyo atauwalilisha mkoa wa Arusha katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa mikoa baadaye mwaka huu.
Hatua ya Sita Bora ya Ligi ya Taifa ngazi ya mkoa wa Arusha itachezwa kwa mkondo mmoja na mechi zote zitafanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa. Kabla ya kupatikana timu sita jumla ya timu 15 zilishiriki hatua ya makundi ya ligi ya taifa ngazi ya mkoa wa Arusha na kila kundi lilitoa timu mbili.

No comments