Update:

01 March 2017

JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LIMEFANIKIWA KUKAMATA SILAHA ZILIZO KUWA ZIKITUMIKA KATIKA KUFANYIA UALIFU NA UJANGILI WILAYANI NGORONGOROJeshi la polisi Mkoani Arusha limefanikiwa kukamata bunduki 10 pamoja na risasi 59 wilayani Ngorongoro ambazo zilikuwa zikitumika katika masuala mbalimbali ya kiuhalifu pamoja na ujangili mkoani hapa.

Akitoa taharifa hizi kwa wandishi wa habari kamanda wa polisi Mkoani wa Arusha kamanda Charles Mkumbo ameeleza kuwa walianza kufanya msako katika kijiji cha Olorien Magaidiru ambapo katika kijiji cha Oldonyosambu waliweza kukamata silaha hizo aina tofauti ambazo zilitekelezwa kichakani.

Mbali na kamanda Mkumbo kuuzungumza hayo pia ameeleza kuwa walifanya mahojiano na viongozi mbalimbali wa kimila wakiwemo Wamasai pamoja na Wasonjo ambapo walieleza sehemu silaha hizo zilikofichwa huku akieleza wasawasi wake kuwapo kwa silaha nyingi zaidi katika jamii hizo.Aidha Kamanda Mkumbo ametoa onyo kali kwa wananchi wote wa Mkoani Arusha wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wazisalimishe mara moja katika ofisi za mtaa au kijiji kwani atakaye kiuka au kupatikana na silaha kinyume cha sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ambapo silaha hizo zimekuwa zikitumika katika mambo mbalimbali ya kijangili pamoja na ujambazi.

NA: ANNA MCHOME