Update:

06 March 2017

IGP aagiza polisi wasiofuata sheria wafukuzwe kazi

Mkuu wa jeshi la polisi Inspekta jenerali ERNEST MANGU amewaagiza makamanda wa polisi wa mikoa kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafukuza kazi askari polisi yeyote atakayebainika kukwamisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

MANGU ameyasema hayo mkoani mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi na kuwataka makamanda hao kufichua askari polisi wanaoshiriki kwenye vitendo vya uhalifu ikiwemo rushwa na biashara haramu  ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

MANGU pia ameagiza kuimarishwa kwa msako dhidi wafanyabiashara na watumiaji wa pombe kali zilizofungashwa kwenye mifuko ya plastiki maarufu kama viroba.