Update:

01 March 2017

Ekari sita za Bangi zateketezwa RuvumaWatu wawili wamekamatwa mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kulima ekari sita na nusu za bangi .


Kamanda wa polisi wa mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi, Zuberi Mwombeji amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika kijiji cha Likunga kata ya Lusewa wilaya ya Namtumbo ambapo bangi hiyo imeteketezwa.


Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mawazo Ngonyani na Thabit Jafari.


Mara baada ya kukamata bangi hiyo jeshi la polisi liliteketeza shamba hilna kuwataka wananchi ambao wanajihusisha na kilimo hicho kujisalimisha polisi