Update:

Boda boda yaendeleza ubabe ligi ya Mkoa wa Arusha

Ligi ya Taifa Ngazi ya Mkoa wa Arusha imeendelea kutimua vumbi katika uwanja wa kumbukumbu ya Shekh Amri Abeid Mjini Arusha.
 Domingo kutoka wilayani Arumeru imetoshana nguvu zidi ya Bodaboda ya Karatu, Timu hizo zilitoshana nguvu lakini Domingo ina kila sababu za kujilaumu zaidi kwa kukosa nafasi nyingi za wazi
Kwa matokeo hayo  Domingo wanafikisha Point 5 mara baada ya kucheza mechi tatu huku Timu ya Bodaboda kutoka Karatu ikiendelea kuongoza ligi hiyo kwa kufikisha point 7  mara baada ya michezo mitatu
 Ligi hiyo inataraji kutimua vumbi hapo kesho kwa mchezo mmoja baina ya Arusha meat  Vs Hobby ya Arumeru mchezo utakao anza mishale ya ya saa 16;00 jioni  katika viwanja vya Shekh Amri Abeid Stadium.
Mwandishi:Clement Shari

No comments