Update:

Binti ajiuwa kwa kujitupa katika ziwa Masila kijiji cha Kirwavunjo Mkoani Kilimanjaro

Binti mmoja anayesadikika kuwa na umri kati ya miaka 16-17 ahofiwa kufa maji baada ya kujirusha ndani ya ziwa masila huko kirwavunjo mkoni Kilimanjaro
Akizungumza na mwandishi wa sunrise radio suhuda wa tukio hilo anasema binti huyo ambaye jina lake halikujulikana amesema binti huyo  alionekana kukimbia na moja kwa moja kujirusha katika ziwa masila ambapo walionekana wamama wawili kummkimbiza ili kuweza kumuokoa maisha yake baada ya kuwatangazia anajiuwa hataki tena kuishi
Aidha ameendelea kusema baada ya binti huyo kujitupa wamama wale walipiga kelele ili wapate msaada lakini hawakuweza kupata msaada wowote na waliendelea kumtafuta Yule dada mda ule bila kumpata
Aidha uongozi wa kijiji cha masila ukishirikiana na wananchi pamoja na familia ya binti huyo wanazidi kumtafutaila mpaka sasa hayjapatikana
Aidha mpaka sasa uongozi pamoja na wanakijiji wanazidi kumtafta na kutoa rai kwa wananchi wote au kwa yoyoyte ataefanikiwa kumuona au kuuona mwili wa binti huyo kutoa taarifa.
Na Anna Mchome 

No comments