Update:

Ajikata uume wake kwa kisu na kumpa mbwa, adai kuwa hauna umuhimu kwake

Katika hali ya kushangaza mwanaume mmoja Nchini KENYA ajikata uume wake na kumpa Mbwa Adai kuwa kiungo hicho hakina thamani na umuhimu wowote kwake.
Majirani walifika katika chumbani mwa mwanaume huyo baada ya kusikia akipiga kelele zinzoashiria  kulia kwa uchungu ambazo ziliwapelekea majirani hao kwenda kujua kilichomsibu ili waweze kumsaidia.
Mmoja wa mashuhuda alisema kuwa alimkuta Mwanaume huyo akiwa nusu uchi huku akivuja damu nyingi huku akiwa tayari ameshaukata uume wake.
Baada ya majirani kufika na kujua kilichotokea walimkimbiza Mwanaume huyo katika hospitali ndogo katika Kaunti ya Naivasha kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

No comments